MAJUKUMU YA KITENGO CHA MAENDELEO YA UFUGAJI WA NYUKI.
Kutekeleza Sera, Sheria, Kanuni na miongozo ya sekta ya ufugaji wa Nyuki
Kuhakikisha Nyuki na rasilimali zake zinahifadhiwa na kutumika katika misingi endelevu
Kushiriki katika tafiti na kutafsiri matokeo ya tafiti yanayohusiana na shughuli za kiuchumi zinazotokana na sekta ya ufugaji wa Nyuki
Kuhamasisha uhifadhi endelevu wa maeneo ya kufugia Nyuki
Kutoa mafunzo kwa wafugaji Nyuki/Jamii juu ya mbinu bora za ufugaji wa Nyuki kwa ajili ya kuboresha uchumi na hifadhi ya mazingira
Kushirikiana na wadau wa sekta mtambuka kuhakikisha uwepo wa masoko ya uhakika ya mazao ya Nyuki pamoja na viwanda vya kuchakata mazao ya Nyuki
Kuishauri Halmashauri juu ya masuala yote yanayohusiana na sekta ya ufugaji wa Nyuki
Kukusanya, kuchakata na kuhifahi takwimu za maendeleo ya ufugaji wa Nyuki
Kushirikiana na wadau kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo ya ufugaji wa Nyuki kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho kiuchumi, mazingira na kijamii
Kudhibiti na kutoa taarifa juu ya magonjwa ya Nyuki
Kuhakikisha viwango vya ubora, usalama na mfumo wa ufuatiliaji wa mazao ya Nyuki vinafuatwa
Kusimamia na kuratibu masuala yote yahusuyo watumishi katika ngazi ya kitengo
Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya ufugaji wa Nyuki zinazotekelezwa na wadau wote katika mnyororo wa Sekta hii
Kuratibu na kutekeleza masuala yote ya maendeleo ya ufugaji wa Nyuki yatakayojitokeza au/na kuelekezwa na Halmashauri
MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KWA KIPINDI CHA 2015/2016 HADI 2020/2021