DAWATI LA MALALAMIKO LA HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA.
Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ni miongoni mwa Halmashauri 8 za Mkoa wa Tabora. Halmashauri ina jumla ya Kata 29, Mitaa 134 na Vijiji 41. Halmashauri imeanzisha Madawati ya Malalamiko kuanzia ngazi ya Halmashauri, Kata, Mitaa na Vijiji. Lengo la madawati haya ni kuimarisha utawala wa kidemokrasia na kuongeza wigo wa kuwasikiliza wananchi katika kupokea maoni na kutatua kero mbalimbali.
Hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora anawatangazia watumishi na wananchi wote kuwa, yeyote mwenye maoni na malalamiko yanayohusu vitendo visivyo vya uadilifu, na rushwa katika huduma zinazotolewa kuwasilisha maoni/malalamiko kwa kufika ofisi ya Mkurugenzi Kitengo cha Malalamiko au kutuma ujumbe mfupi au kupiga simu kwa kutumia namba ifuatayo:
0765 835539 (Dawati la Malalamiko la Halmashauri)
Pia maoni/malalamiko yanaweza kuwasilishwa kwa kutumia barua pepe ya Halmashauri ambayo ni malalamiko@taboramc.go.tz au kujaza fomu maalumu iliyopo kwenye tovuti ya Halmashauri www.taboramc.go.tz
IMETOLEWA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA TABORA
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.