1. UJENZI WA MRADI WA JENGO LA MADUKA ENEO LA PRIME TABORA MJINI
Mradi huu ambao unamba una jumla ya maduka 30 ulianzishwa kutokana na changamoto ya Halmashauri kuwa na Mapato Kidogo kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani, hivyo kuanza kufanya kazi kwa mradi huu kumeiwezesha Halmashauri kuongeza mapato kutokana na Tozo ya pango , Leseni za Biashara, Maegesho ya Magari na Usafi wa Mji.
Shughuli zilizofanyika wakati wa Utekelezaji wa mradi
Halmashauri inatarajia kukusanya Jumla ya TSh. 40,500,000/= ikiwa ni Kodi ya Jengo, Pia Kiasi cha Tsh. 1,260,000/= kimekusanywa ikiwa ni Leseni za Biashara kwa Maduka 18, mradi pia umetoa ajira mbalimbali tangu kuanza kwa ujenzi mpaka kukamilika, mzunguko wa fedha umeongezeka pamoja na mwonekano wa Manispaa kuwa mzuri zaidi
Kupata Taaria zaidi bofya hapo chini.
UJENZI WA MRADI WA JENGO LA MADUKA ENEO LA PRIME TABORA MJINI.pdf
2. UJENZI WA MRADI WA SKIMU YA UMWAGILIAJI BWAWA LA INALA
Mradi wa Skimu ya umwagiliaji Inala ni mradi ulioanzishwa na Kujengwa katika Kijij cha Inala kata ya Ndevelwa ambao umehusisha ujenzi wa Bwawa na Miundo mbinu ya Umwagiliaji ambapo hadi sasa bwawa lina ujazo wa mita za ujazo 1,376,000 ambalo lina uwezo wa kumwagilia eneo la ukubwa wa hekta 400 wakati wote kwa ajili ya kilimo cha mpunga , mahindi na mboga mboga.
Vilevile Halmashauri imefanikiwa kujenga miundo mbinu ya umwagiliaji kufikia hekta 232 na gharama ya mradi huu kwa ujumla ni Tsh. 1,656,342,651.809 ikihusisha ujenzi wa bwawa pamoja na skimu ya umwagiliaji.
Mradi ulianzishwa kwa lengo la kutatua changamoto ya ukosefu au upungufu wa Chakula kwa wakazi wa Manispaa ya Tabora ambao husababishwa na kilimo duni kutokana na Manispaa ya Tabora kutopata mvua za kutosha kuwezesha shughuli za kilimo cha mazao ya chakula kama mpunga na mahindi hivy kuisababishia serikali gharama kubwa ya kutoa chakula cha msaada ili kuokoa kaya ambazo huathirika kutokana na ukosefu wa chakula
Mafanikio ya mradi ni kwamba mpaka sasa wakulima wapatao 400 wamegawiwa mashamba ili kuanza kilimo cha mpunga na inatarajiwa ujenzi wa skimu ukikamilika wakulima wapatao 1000 watanufaika kwa kulima kilimo chenye tija na kupata uhakika wa chakula , kuinua kipato cha wakulima, kukua kwa uchumi katika Manispaa na wakulima waliopo karibu na mradi kupata maji ya kunyweshea mifugo yao.
Wakulima wamepatiwa mafunzo kupitia mashamba darasa yaliyotolewa na Wataalamu kutoka Manispaa ya Tabora kwa Kushirikiana na Wataalamu kutoka Chuo cha Kilimo Tumbi
Kupa Taaria zaidi bofya hapo chini.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Manispaa Tabora, 4 Barabara ya Kiwanja cha Ndege
Anwani ya Posta: S.L.P 174, 45182 Tabora
Simu ya Ofisi: +255 262606088
Simu ya Mkononi: +255
Barua Pepe: md@taboramc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.