• Lalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
TABORA MUNICIPAL COUNCIL
TABORA MUNICIPAL COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Ardhi
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • MIfugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Kata
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Uwekezaji
    • Vituo vya Utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Malalamiko
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi , Elimu na Afya
      • Kamati ya Maadili
      • Ukimwi
    • Ratiba
      • Vikao vya Halmashauri
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu za maombi
    • Miongozo, Sera na Kanuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha

KILA HALMASHAURI IHAKIKISHE IMEPANDA MITI ISIYOPUNGUA MILIONI MOJA NA LAKI TANO

Posted on: November 24th, 2022

Na Alex E. Siriyako;

Maelekezo haya ya Serikali yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batilda S. Buriani leo  Novemba 24, akizindua Kampeni ya upandaji miti katika Mkoa wa Tabora, uzinduzi ambao umefanyika katika kijiji cha Igombe, Kata ya Kabila, Manispaa ya Tabora.

Uzinduzi huu wa Kimkoa unafuata baada ya Uzinduzi wa Kitaifa ambapo kila Mkoa ulipewa Malengo ambayo vilevile yalivunjwavunjwa hadi kufikia hatua ya Halmashauri ambapo kila Halmashauri inatakiwa kupanda miti isiyopungua milioni moja na laki tano kwa mwaka.

Katika uzinduzi huu ambao umeratibiwa na Tanzania Forest Services (TFS), taasisi za Umma na mashirika yasiyo ya Kiserikali nayo yameshiriki mathalani mabenki, TANESCO, Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi, Manispaa ya Tabora, pamoja na wadau wengine wa mazingira wakiwamo Wananchi wa Kata ya Kabila.

Mkuu wa Mkoa katika hotuba yake amemshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayofanya ya kuleta fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo lakini pia kwa jitihada zake za makusudi za kupambana na changamoto na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema Serikali inaendelea kupambana kuhakikisha kwamba gesi ya kupikia majumbani inapatikana kwa bei ya chini sana kiasi cha kumfanya mwananchi wa kawaida asiwe na ulazima wa kutumia mkaa na kuni, kwani kwa hatua hiyo tutapunguza mahitaji ya mkaa hususani mijini na tutalinda misitu yetu.

Aidha katika hotuba yake, Mkuu wa Mkoa ametumia wasaa huo kuwataka Wanachi wa Vijiji vya Ukumbi Kakonko na Usinga vilivyopo katika hifadhi ya mto Igombe katika Wilaya ya Kaliu waondoke kwa hiari mapema iwezekanavyo kabla Serikali haijaamua kutumia nguvu kuwatoa katika maeneo hayo. Na kwa msisitizo Dkt. Batilda ametanabaisha kuwa shughuli za kilimo zinaruhusiwa kufanyika kuanzia mita 300 kutoka chanzo cha maji hususani kwa wale wanaopakana na vyanzo vya maji.

Katika kuhitimisha hotuba yake, Mhe. Batilda amewataka Mamlaka ya kuhifadhi Misitu Tanzania (TFS) kwenda kwenye vyombo vya habari kuelimisha Umma wa Watanzania kuhusu sharia  dhidi ya ukataji miti kiholela, sharia za Kudhibiti uharibifu wa Mazingira ikiwa ni pamoja na kueleza adhabu anazoweza kukabiliana nazo mtuhumiwa pindi akikamatwa na vyombo vya usalama.

Nae Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Mhe. Ramadhani Kapela amepata fursa ya kutoa salamu kwa hadhara hiyo, ambapo amemshuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia S. Hassan kwa fedha vyingi sana za miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Tabora hususani sekta ya Elimu, Afya na Barabara.

Matangazo

  • TANGAZO LA MAFUNZO YA KILIMO KWA VIJANA PROGRAM YA BBT January 13, 2023
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA KATIKA ENEO LA TULI KATA YA IFUCHA - INALA July 25, 2022
  • TANGAZO KWA WANANCHI NA TAASISI WALIOOMBA VIWANJA KATIKA ENEO LA INALA - TULI August 17, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2023 - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA December 14, 2022
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WALIMU 1680 WA MANISPAA YA TABORA WAPATA VISHIKWAMBI

    January 24, 2023
  • WARATIBU ELIMU KATA WASAINI MIKATABA YA MPANGO WA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UBORESHAJI NA USIMAMIZI WA ELIMU KWA MWAKA 2023

    January 20, 2023
  • ALAT MKOA WA TABORA WARIDHIKA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO YA MANISPAA YA TABORA

    January 14, 2023
  • RAIS WA JAMHURI YA TANZANIA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ATOA ZAWADI YA KRISMASI

    December 24, 2022
  • Angalia Zote

Video

TAARIFA YA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AGOSTI 14, 2022 TABORA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Jarida la Halmashauri Julai - Septemba 2022
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri 2021/22 - 2025/26
  • Capital Investment Plan
  • Tabora Master Plan 2015 - 2035
  • eMrejesho ( Kutuma, kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi)
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Fursa za Uwekezaji
  • Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma

Kurasa Zinazofanana

  • IKULU
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mkoa wa Tabora

Waliotembelea Tovuti

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.