• Lalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
TABORA MUNICIPAL COUNCIL
TABORA MUNICIPAL COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango Miji na Ardhi
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • MIfugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Kata
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Uwekezaji
    • Vituo vya Utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Malalamiko
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi , Elimu na Afya
      • Kamati ya Maadili
      • Ukimwi
    • Ratiba
      • Vikao vya Halmashauri
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu za maombi
    • Miongozo, Sera na Kanuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha

MANISPAA YA TABORA YANG’ARA KIMKOA KATIKA UJENZI WA MADARASA YA KIDATO CHA KWANZA

Posted on: November 21st, 2022

Na Alex Siriyako;

Manispaa ya Tabora ni moja ya Halmashauri nane za Mkoa wa Tabora ambazo zote ziko kwenye utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2023, ambapo Mkoa wa Tabora pekee una madarasa 565. Manispaa ya Tabora ambayo inajenga madarasa 69, imeongoza katika kasi ya ujenzi wa madarasa hayo katika Mkoa wa Tabora.

Taarifa hii imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Angellah Kairuki katika majumuisho ya Ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Tabora yaliyofanyika Ziba, Wilaya ya Igunga, ambapo amekagua ubora na kasi ya ujenzi wa madarasa ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023, lakini pia amekagua Shule zilizojengwa kwa fedha za mradi wa SEQUIP ambapo shule hizo nazo zinatarajia kupokea wanafunzi mwaka ujao wa 2023.

Waziri Kairuki amesisitiza Viongozi wote kwa nafasi zao waendelee kufuatilia miradi hii kwa ukaribu sana na akasisitiza kasi ya ujenzi wa madarasa haya iongezeke ili kufikia lengo la Serikali la kuhakikisha mpaka kufikia Desemba 15, mwaka huu ujenzi uwe umekamilika.

Aidha Mhe. Kairuki amesisitiza taratibu za manunuzi ya Umma zifuatwe katika manunuzi yote ya bidhaa za ujenzi wa madarasa haya pamoja na miradi mingine yote ya Serikali. Waziri amesisitiza uaminifu sana na kuepuka asilimia kumi kwa wazabuni kwani vitendo hivi vya kifisadi vinazorotesha kuanzia ubora wa miradi mpaka kasi ya utekelezaji.

Mhe. Kairuki amewaonya Wafanyabiashara wanaoficha bidhaa za ujenzi ili ziadimike na kupandisha bei ya bidhaa hizo mathalani simenti na nondo, kwamba huo ni uhujumu uchumi na ameagiza Vyombo vya Dola viendelee kufuatilia watu hao na hatua za kisheria zichukuliwe pindi wanapobainika.

Wakati huohuo Mhe. Kairuki amewaomba Wananchi waendelee kuweka mchango wao mathalani nguvu kazi katika ujenzi wa miradi ya Serikali ili kuwezesha miradi hiyo kukamilika kwa ubora uliokusudiwa kwani maeneo mengi Nchi hii yanatofautiana na hivyo kuna baadhi ya maeneo fedha zinakuwa hazikidhi mahitaji, hivyo nguvu ya Wananchi inapoongezeka miradi hukamilika kwa ubora wake.

Katika maelekezo yake wakati wa majumuisho haya, Mhe.Waziri amewataka Wakurugenzi wawajengee uwezo ikiwa ni pamoja na mafunzo ya kozi za muda mfupi mafundi wanaojenga miradi ya Serikali kwa mfumo wa Force Account, kwani mafundi hawa hususani ambao wanafanya vizuri kuna haja ya kuwapa mafunzo ili waendelee kufanya vizuri Zaidi.

Matangazo

  • TANGAZO LA MAFUNZO YA KILIMO KWA VIJANA PROGRAM YA BBT January 13, 2023
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA KATIKA ENEO LA TULI KATA YA IFUCHA - INALA July 25, 2022
  • TANGAZO KWA WANANCHI NA TAASISI WALIOOMBA VIWANJA KATIKA ENEO LA INALA - TULI August 17, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2023 - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA December 14, 2022
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WALIMU 1680 WA MANISPAA YA TABORA WAPATA VISHIKWAMBI

    January 24, 2023
  • WARATIBU ELIMU KATA WASAINI MIKATABA YA MPANGO WA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UBORESHAJI NA USIMAMIZI WA ELIMU KWA MWAKA 2023

    January 20, 2023
  • ALAT MKOA WA TABORA WARIDHIKA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO YA MANISPAA YA TABORA

    January 14, 2023
  • RAIS WA JAMHURI YA TANZANIA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ATOA ZAWADI YA KRISMASI

    December 24, 2022
  • Angalia Zote

Video

TAARIFA YA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AGOSTI 14, 2022 TABORA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Jarida la Halmashauri Julai - Septemba 2022
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri 2021/22 - 2025/26
  • Capital Investment Plan
  • Tabora Master Plan 2015 - 2035
  • eMrejesho ( Kutuma, kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi)
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Fursa za Uwekezaji
  • Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma

Kurasa Zinazofanana

  • IKULU
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mkoa wa Tabora

Waliotembelea Tovuti

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.Haki zote zimehifadhiwa.